Wabunge watakiwa kuwahamasisha wananchi kutokomeza Kifua Kikuu nchini

Wabunge watakiwa kuwahamasisha wananchi kutokomeza Kifua Kikuu nchini

Hayo yameelezwa na mbunge wa viti maalumu (CCM) Mh. Najma Giga aliyemuwakilisha Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai katika uzinduzi wa mtandao wa wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.

Mhe. Giga amesema kuwa ni wajibuwa kila mbunge nchini kuisimamia serikali ili ishughulikie kikamilifu tatizo la kifua kikuu kwa kutenga rasilimali za kutosha kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo hatari.

“Kifua kikuu kinaleta madhara kiafya na huongeza umasikini katika jamii, takribani watu 154,000 uugua kila mwaka na 27,000 ufariki duniani ikiwa ni sawa vifo 74 kwa siku, hii inaonesha ni jinsi gani ugonjwa wa TB ni hatari na hivyo juhudi za ziada zinahitajika ili kuutokomeza”. Amesema Mh. Giga.

Aidha Mh. Giga ameipongeza serikali na wataalamu wa afya kwa kuweza kuchunguza na kutoa matibabu kwa wagonjwa wa kifua kikuu na kuhakikisha wagonjwa wanapata matibabu bure na wanapona kabisa katika hospitali zote nchini.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa taarifa juu ya jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali katika kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu mbele ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Mh. Najma amesema kuwepo kwa mtandao wa wabunge wa kupambana na TB nchini (Parliamentary TB Focus) kutawezesha kufikia malengo ya kimataifa na kitaifa ya kutokomeza TB kwa kutambua kuwa ni janga la kitaifa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema wizara hiyo inatoa kipaumbele juu ya ugonjwa wa TB kwa kufanya juhudi kubwa ya kuutokomeza ugonjwa huu nchini ikiwemo kuweka teknolojia za kisasa za mashine za Genex part zaidi ya 209.

“Jambo ambalo tumelifanya kama serikali ni kujaribu kufanya utaratibu tofauti wa jinsi gani ya kufanya upimaji wa ugonjwa huu. Hadi hivi sasa tumeweka teknolojia za kisasa za mashine za Genex part zaidi ya 209 nchi nzima ambazo utoa majibu ndani ya masaa mawili”. Alisema Dkt. Ndugulile.

Pia Dkt. Ndugulile amesema kuwa dawa zote zinazotibu kifua kikuu cha kawaida na kifua kikuu sugu zinapatikana nchini na matibabu yake pamoja na vipimo vyote vinavyohusiana na ugonjwa wa TB yanatolewa bure.

Sambamba na hayo, Shuhuda Bi. Agatha Chikoti aliyewahi kuugua ugonjwa wa kifua kikuu ameiasa jamii kuacha kwenda kutafuta dawa za kienyeji na badala yake kwenda hospitali kupima na kupewa tiba sahihi.

“Picha ya Pamoja ikiongozwa na Mgeni rasmi ambae ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mh. Najma Giga aliyemuwakilisha Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai katika kikao cha Uzinduzi wa Mtandao wa Wabunge duniani wenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu uliofanyika katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.”

Author: admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *